Kijana mmoja ameingia kwenye mtandao wa Twitter kueleza hali iliyompelekea kukatisha uhusiano wake na mpenzi wake kisa kuomba pesa ya akwenda kusuka.
Kijana huyo anayejulikana kwa jina la @ArtificialSteez kwenye Twitter, alisema kuwa gari lake lilipata ajali, hivyo alilazimika kulipia gari jingine kwa muda, huku akijaribu kurekebisha lililoharibika na alisema kuwa kampuni ya bima isingewezakugharamia matengenezo kwa sababu si yeye aliyekuwa akiendesha gari wakati ajali hiyo ilipotokea.
Hata hivyo, mpenzi wake alimwomba pesa kwa ajili ya nywele zake siku iliyofuata, lakini hakuweza kumpatia, kwa hiyo alikasirika na ulipotokea ugomvi aliamua kuachana nae kwa sababu ya kile alicho dai kuwa mwanamke huyo hajali kwani aliwahi kumlalamikia kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kutokana na kutafuta pesa za kurekebisha gari.
Aliandika, “Gari langu lilipata ajali, na ilinibidi kulipia gari la muda kisha nikamwambia nina stress na pesa za kurekebisha gari kwani bima haitanilipa kwa sababu rafiki yangu alikuwa akiiendesha. aliniomba pesa za nywele siku moja baadaye na nilikasirika sikuweza kwasababu sikuweza kumpa 💀💀”
My car was in an accident n I had to pay for a temporary car then told her I’m stressed about money to fix the car since insurance won’t pay cuz my friend was driving it.
— Lil Fish🎣 (@ArtificialSteez) July 25, 2023
She asked me for hair money a day later n was upset I couldn’t do it💀💀 https://t.co/SQWVlaIzPJ