Stori Kubwa

Stori kuhusu Mtoto wa miaka minne alivyompiga risasi mdogo wake

on

BASTOLA3

Ni nadra sana kwa hapa kwetu kuona bastola zikitumika kirahisi ndani ya familia,lakini kwa wenzetu ni jambo la kawaida ambalo unaweza kulifananisha kama kumiliki simu ya mkononi ambayo unaweza kuiacha sehemu yoyote.

Huko nchini Marekani mzazi aliamua kuiacha bastola yake kitandani bila kujali kuwa ana watoto wadogo ambao hawakua na uelewa na silaha hiyo baada ya kuichukua na kuanza kuichezea.

Habari kutoka Ohio nchini Marekani zinasema tukio hilo limetokea wakati Watoto hao wakiwa wanacheza peke yao ndani ya chumba ndipo Mtoto huyo aliposhika Bastola hiyo na kumjeruhi mdogo wake kichwani.

Taarifa za Polisi zinasema Baba wa Mtoto huyo alikuwa amembeba Mtoto huyo aliyejeruhiwa  wakati Polisi walipofika eneo la tukio huku Kaka yake akilia na kuwaomba askari hao msamaha mara kwa mara.

Kamanda wa Polisi Roger Watkings amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kuona kama linaweza kuwa kosa la jinai ama vinginevyo.

Source NTNNews

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

 

Tupia Comments