Vituko/ Comedy

Pale ambapo unaamua kuyajaribu maumivu ya risasi kwenye mwili wako mwenyewe !!

on

IMGKesi za watu kujipiga risasi ni ishu ambazo ziko kwenye headlines.. zimekuwa zikitokea sehemu mbalimbali duniani kutokana sababu mbalimbali.

Hii imetokea Hispania.. jamaa kakaa akaona ajaribu kujipiga risasi ili aone tu maumivu yake yakoje… baada ya kupata jibu akachukua maamuzi mazito, kachukua bastola yake akajipiga mguuni.

Polisi hawakumuacha, alitangulizwa kwanza hospitali, akapewa matibabu alafu ishu ikahamia kwenye meza ya Mahakama.

Jamaa huyo alijitetea kwa polisi  kuwa aliamua kufanya kitendo hicho ili kujua mtu anayepigwa risasi huwa anajisikiaje maumivu yake.. upepelezi unaendelea juu ya kesi.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments