Mazishi ya Mzee Gurumo yamefanyika leo katika kijiji cha Masaki kilichopo wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani ambako mamia ya watu yalikusanyika kumsindikiza kwenye safari yake ya mwisho.
Miongoni mwa watu waliohudhuria mazishi haya ni pamoja na Wasanii Ally Choki, Super Nyamwela,Mzee Zahir Zoro,Profesa Jay na wanamuziki wengine wa band mbalimbali Tanzania.