Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa rai kwa dunia kuchukua hatua sasa ili kuilinda na kuienzi rasilimali maji kwa ajili ya kizazi hiki na mustakbali wa kizazi kicjacho wakati huu rasilimali hiyo ikizidi kuwa adimu.
Kupitia ujumbe wake wa siku ya maji duniani inayoadhimishwa kila mwaka Machi 22 Guterres amesema Mahitaji ya wanadamu ya maji yanaongezeka.
Shinikizo juu ya rasilimali za maji zinaongezeka kutokana na matumizi makubwa, uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
Ukame na mawimbi ya joto yanazidi kuwa makali na ni mara kwa mara kwa kupanda kwa kina cha bahari kunasababisha kuingiliwa kwa maji ya chumvi kwenye chemichemi za pwani na maji ya chini ya ardhi nayo yanapungua.
Ameongeza kuwa maji yanaweza kuwa chanzo cha migogoro lakini pia cha ushirikiano.
amesisitiza “Ni muhimu kwamba tufanye kazi pamoja ili kutoa usimamizi bora wa vyanzo vyote vya maji, ikiwa ni pamoja na usambazaji wa maji ya chini ya ardhi duniani, maji ya ardhini hayaonekani, lakini hatuwezi kumudu kuyasahau yakiwa yamehifadhiwa kwenye miamba na udongo, maji ya chini ya ardhi ndio chanzo chetu kikubwa cha maji safi.
Hata hivyo, asilimia 20 hivi ya chemichemi za maji duniani zinatumiwa kupita kiasi hatujui thamani halisi ya maji.
Hivyo amehimiza “Katika siku hii ya maji duniani, tujitolee kuimarisha ushirikiano kati ya sekta na kimataifa ili tuweze kuleta uwiano baina ya mahitaji ya watu na asili na kutumia maji ya ardhini kwa vizazi vya sasa na vijavyo.”