Leo March 7, 2018 Inaelezwa kuwa asilimia 30 na 40 ya wagonjwa wote waliolazwa kwenye wodi ya wanawake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni wanaougua magonjwa ya saratani ya shingo ya kizazi.
Haya yameelezwa hivi karibuni na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake katika hospitali ya Muhimbili Vincent Tarimo alipozungumza na moja ya chombo cha habari nchini na kueleza kuwa ugonjwa huo huendana na magonjwa ya figo.
Dk. Tarimo ameeleza kuwa wanawake wanaougua magonjwa ya figo hukumbwa pia na matatizo ya uzazi, hasa kushindwa kushika mimba na baadhi ambao hubahatika kushika mimba, basi mimba hizo hutoka kabisa.
Hali hiyo ikitokea Dk. Tarimo ameeleza kuwa madaktari huamua kukomaza watoto ikiwa mwanamke anakaribia wakati wa kujifungua au kuamua kuharibu mimba hiyo ili kwamba kuokoa figo za mama.
Mbunge alivyoongoza Wananchi kuua Tumbili Jimboni
Waajiri 6907 DSM kupelekwa Mahakamani