Serikali ya China iko kwenye maandalizi ya kutengeneza treni yenye mwendokasi wa juu zaidi kuliko zote duniani ambayo itasafiri katika barabara za juu za treni yaani flyover na itakuwa na uwezo wa kusafiri kwa umbali wa kilometa 4000 kwa saa ikisafirisha abiria na mizigo.
Umbali huu wa kilometa 4000 ni sawa na umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Afrika Kusini ambapo treni hii itachukua saa moja tu kukamilisha umbali huo. Wakala wa utekelezaji wa treni hiyo waitwao ‘China’s Aerospace Agency’ wanaendelea na utafiti juu ya mradi huo.
Kwa mujibu wa Rais wa China Xi Jinping ameeleza kuwa japokuwa mradi huo ambao ni wa mabilioni ya pesa utakua mradi mkubwa kushinda miradi yote mikubwa ya usafirishaji duniani, pia mradi huu utavunja rekodi ya karne.
Ulipitwa na hii? BREAKING: Madini ya BILIONI 32 yazuiwa Airport DSM
UNATAKA KUANZISHA KIWANDA? Kuna hii ya fahamu kutoka TPSF