BreakingNews

BREAKING NEWS: Inayomuhusu Askofu Gwajima kutoka Polisi Central jioni hii

on

Ni kutoka kwenye headlines za sakata la dawa za kulevya kupitia kwenye orodha aliyoitaja Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye awamu ya pili ambayo ilijumuisha majina ya watu 65 akiwemo Askofu Gwajima.

Kutoka Kituo cha Polisi Kati Dar es salaam jioni hii, camera ya AyoTV imemnasa Askofu huyo wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima akiwa anatoka kwenye kituo hicho cha Polisi alikokua ameshikiliwa toka Alhamisi kufuatia kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda.

Baadhi ya Waumini wa Kanisa lake walikua nje ya kituo hicho cha Polisi jioni hii na walisikika wakizungumza maneno mbalimbali ya kushukuru kama vile “Asante Yesu”

Video ya tukio lenyewe itafata hivi punde kupitia hapahapa millardayo.com na Youtube ya Millard Ayo, hakikisha umekaa karibu yangu kwenye FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM, SNAPCHAT na APP kwa jina hilohilo la “millardayo” kwenye Android na IOS ili kupata kila BREAKING NEWS papohapo.

ULIPITWA? Alichosema Gwajima baada ya kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa mkoa Paul Makonda kipo kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments