Mix

VideoFUPI: Askofu Gwajima aeleza kilichotokea alipokuwa Polisi

on

Baada ya jana Feb. 11 Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima kuachiwa na Polisi baada ya mahojiano yaliyodumu toka Alhamisi kituo cha Polisi kati Dar es salaam kufuatia sakata la dawa za kulevya, leo February 12 2017 akiwa kwenye Ibada kanisani kwake amesimulia.

‘Nilienda moja kwa moja kwa Kamanda Sirro, nikamkuta na Manji, wakasema wewe na Manji tunakwenda kuwapima kwa mkemia mkuu wa Serikali, wale watu waliokuwa wanapima walikuwa wanapima kwa uwazi kabisa, wakapima vitu vyote majibu hamna chochote’-Askofu Gwajima

Waliposema twende tukapime nilikua tayari, na mimi nilisema ndani yangu hata ukiona Pombe andika umeona dawa za kulevya, nikasema mimi sina tatizo twendeni nyumbani kwangu na mkikuta hata sigara andikeni ni dawa za kulevya, wakasachi na hawakukuta kitu”

VIDEO: Alichoongea Askofu Gwajima kwa mara ya kwanza toka alipotajwa kwenye orodha ya dawa za kulevya ya Paul Makonda, bonyeza play kwenye hii video hapa chini

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako Millard Ayo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments