Siku chache baada ya aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa kutangaza kwamba ameamua kuachana na Siasa, hiyo ilikuwa siku kadhaa baada ya Dk. Slaa kutoonekana kwenye Mikutano pamoja na Vikao vya CHADEMA pamoja na Vyama vya UKAWA, stori ambazo zinamtaja yeye bado hazijaacha kuibuka.
Kulikuwa na madai ambayo yaliripotiwa na Vyombo vya Habari pamoja na kuandikwa sana Magazetini na Mitandaoni pia ambapo Maaskofu walitajwa kuhusishwa na Rushwa… Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima kaongea Dar es Salaam… kwenye alichokisema kuna hizi nukuu za alichokisema pamoja na pichaz pia.
Mchungaji Askofu Josephat GWAJIMA ameongea na Waandishi wa Habari Dar #SEPTEMBER082015, nakusogezea #TWEETS za nukuu kile alichokisema.
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Lengo ni kufafanua maneno yaliyosemwa na rafiki yangu Dk.Wilbrod SLAA na kurushwa karibu kwenye TV zote’-#AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Kati ya maneno yaliyonigusa ni kusema “GWAJIMA aliniambia Maaskofu walipewa Rushwa ili kumsapoti LOWASSA”-#AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Mara nyingi ananitaja mimi kuwa ni rafiki yake, siwezi kumkana kwa kuwa amekosea, ni rafiki aliyekosea’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Urafiki wangu na Dk. SLAA ulianza akiwa CHADEMA ktk Harakati za Ukombozi kuitoa nchi ktk matatizo’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Alipata matishio mengi ya kuuawa na kukamatwa, akaomba nimsaidie kumpa watu salama wa kumsaidia’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Nilimpa Walinzi wanne wa kumlinda, aliogopa kulindwa na Polisi au watu wengine angesalitiwa’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Nilimpa Walinzi waaminifu waliokuwa wananilinda mimi, wamemlinda kwa zaidi ya miaka minne’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Nilimpa na mtu mwingine, mama mtu mzima wa miaka 50 akawa anampikia chakula nyumbani kwake’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Nitakayoongea kuhusu Dk. SLAA nayajua kuanzia jikoni, chumbani na ni ya uhakika kabisa’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Dk. SLAA alisema amehama CHADEMA kwa sababu ya ujio wa LOWASSA, sio kweli’- ‘- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Ujio wa LOWASSA ulianza na Dk. SLAA mwenyewe, alikuja kuniomba nimsaidie wampate LOWASSA ili washinde Uchaguzi ‘- #AskofuGWAJIMA #UPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Mimi siko Kamati Kuu CHADEMA lakini niliomba niingie Kikao cha Kamati Kuu ili kuhakikisha LOWASSA amefika salama’- #AskofuGWAJIMA #UPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Tulimaliza Kikao na SLAA saa sita usiku, baadaye nikaambiwa na Walinzi kuwa mke wa SLAA alimfungia nje’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Nilienda kwa SLAA akaniambia ameamua kujitoa kwenye Siasa kwa sababu Familia yake inavunjika’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Dk. SLAA alikuwa Padri hana uzoefu wa Ndoa, angalau sisi Wachungaji tunajua namna ya kuongoza ndoa’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Niliongea sana na mke wa SLAA amruhusu mume wake aendelee lakini aligoma’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Dk. SLAA alisema kwenye Mkutano CHADEMA watu waliletwa na malori,mlioenda mtajibu kama SLAA ni mkweli au muongo’- #AskofuGWAJIMA #UPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘SLAA amesomeshwa na Kanisa Katoliki, leo anasingizia Maaskofu 30 wamepewa Rushwa ili waonekane hawafai”- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Mimi ninasema Maaskofu wote hawakupewa Rushwa na hata mimi sikupewa’- #AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Alisema kuna wakati nilizunguka na LOWASSA kwenye Ndege, nina Ndege yangu na ninaweza kupakia mtu yoyote’-#AskofuGWAJIMA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘Anayemwongoza SLAA kutukana Maaskofu akome, kama watu wa Usalama mtaruhusu aendelee kutukana mimi nitakaa nae’- #AskofuGWAJIMA #UPDATES — millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
‘SLAA alikuwa Padri, akaacha na kuoa, akiongea tena nitataja watoto wake ambao amewatelekeza na kuoa mke wa mtu’- #AskofuGWAJIMA#UPDATES
— millard ayo (@millardayo) September 8, 2015
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos