Staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo anaweza kukumbana na adhabu kali kutoka chama cha soka cha Hispania kwa kosa la kumsukuma refa Ricardo de Burgos wakati wa game ya Super Cup ya Real Madrid dhidi ya Barcelona.
Ronaldo alioneshwa kadi ya pili ya njano baada ya kujiangusha ndani ya 18, kitendo ambacho kinatafsirika kumdanganya muamuzi na kutokana tayari alikuwa ameonesha kadi ya kwanza ya njano dakika ya 80 kwa kushangilia kwa kuvua jezi uwanjani baada ya kufunga, refa akampa kadi ya pili ya njano ambayo ni red card.
Baada ya dakika ya 82 Ronaldo kuoneshwa kadi ya pili ya njano ambayo ilipelekea aoneshwe red card, alipandwa na jazba na kumsukuma refa wa game hiyo ambayo ilimalizika kwa Real Madrid kupata ushindi wa 3-1 wakiwa ugenini Nou Camp, kwa mujibu wa kanuni za FA ya Hispania kifungu namba 96 Ronaldo anaweza kufungiwa mechi kati ya nne au hadi 12.
https://youtu.be/xY-WHYOWvN4
Alichokiagiza waziri Mwakyembe baada ya kutangazwa matokeo ya Urais na makamu TFF