Habari za Mastaa

“Sijaathirika peke yangu na Seduce Me” – Wema Sepetu

on

Miss Tanzania 2006 ambaye pia ni mwigizaji wa Filamu kutoka Bongomovie Wema Sepetu ni miongoni mwa mastaa wa Bongo ambao wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu wimbo mpya wa mwimbaji Alikiba ‘Seduce Me’ ambao ameutambulisha August 25, 2017.

Kupitia Instagram yake Wema Sepetu ameandika maneno haya>>>”I have something to tell Alikiba… Baba Tunashukuru kwa Mziki mzuri, unatukomesha sana… Unatupa shida masaa yote nyimbo inakuwa kwenye Repeat.

“Yaani sijioni naskiza nyimbo nyingine zaidi ya #SeduceMe … @elizabethmichaelofficial Najua nimesema nyimbo ila ushanielewa ??.. Na ninatambua kwamba hili ni janga letu sote… Sijaathirika peke yangu na Seduce Me…. Kwa mara nyingine tena natoa shukran zangu za dhati kabisa kwako Bwana Bichwa… ??????”

WEMA SEPETU: “Kiba na Diamond ni wendawazimu, wananiudhi” 

Soma na hizi

Tupia Comments