Habari za Mastaa

R. Kelly amaliza deni la matunzo ya Watoto wake mbele ya Mahakama

on

Inaripotiwa kuwa mwimbaji R. Kelly alishinda mahakamani nusu siku kwa ajili ya kukamilisha madai mawili ikiwemo kujibu kwa nini alishindwa kufika mahakamani kwenye shauri lake la kwanza la unyanyasaji wa kingono na pili shtaka la kutoa matumizi ya watoto wake.

Inaelezwa kuwa R.Kelly alikuwa atumikie kifungo cha miaka kadhaa jela kwa kushindwa kulipa fedha za matunzo ya watoto wake watatu kwa mkewe wa zamani Andrea Kellz, ndani ya Mahakama siku ya May 8,2019 R. Kelly  alilazimika kutoa kiasi cha dola 162,000 za Kimarekani sawa na shilingi Milioni 373 za Kitanzania na kumaliza deni hilo la miezi mitatu.

Pia imekuwa ikielezwa kuwa R.Kelly humlipa Andrea Kellz kiasi cha shilingi milioni 46 za Kitanzania kila mwezi. Kutokana na shtaka la kwanza la kushindwa kufika mahakamani, wakili alimtetea kuwa R. Kelly alifikishiwa wito akiwa jela na hakuweza kuusoma kwa sababu ana matatizo ya usomaji.

VIDEO: Umepitwa na hii kutoka kwa Ommy Dimpoz bado anajiuliza “Ni mimi kweli?”, RIP Dr. Mengi, Bonyeza PLAY hapa chini kwa kutazama mwanzo mwisho.

Soma na hizi

Tupia Comments