Makumbusho ya Taifa la Tanzania kupitia kituo chake cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na program ya Sanaa na wasaani yaani Museum Art Explosion kwa kushirikiana na Tabasamy PR Consulty imeandaa Usiku wa Kahawa kwa mwaka huu
2022.
Tukio hilo litafanyika ljumaa Desemba 30, katika jukwaa (threatre) la Makumbusho na na Nyumba ya Utamaduni chini ya kauli mbiu ya African Vintage. Lengo kuu la hafla hiyo ni kuzindua EP (Extended Playlist) ya ‘G3’ ya Gynah (Regina Beraldo Kihwele), mtunzi wa nyimbo ya ‘it’s You”. Gynah ni mwimbaji wa kimataifa, mtunzi wa nyimbo, mwigizaji, mwanamitindo na mwanaharakati wa masuala ya aíya ya akili aliyezaliwa na kukulia jijini Dares Salaam.
Pamoja na kuimba Gynah, ni mbunifu wa nembo ya Kahawa by Gynah, mavazi ambayo yamechangiwa sana na mitindo ya zamani na mguso wa Kiafrika unaochochewa na vitambaa vinavyozalishwa Tanzania ikiwemo Batik, kanga n.k. Kulingana na Gynah,
“Jina la Kahawa limetokana na kinywaji ninachokipenda sana ambapo nikibuni mitindo ama kwenye uandishi wa filamu ama nyimbo huwa natumia kinywaji hiki cha kahawa;
na ndipo nilipofikia maamuzi ya kupatia nembo yangu ya ubunifu jina la kahawa.
Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni imekuwa ikiendesha programu maridhawa ya kila ijumaa ya mwisho wa mwezi ya Museum Art Explosion kwa muda miaka sita sasa lengo lake ikiwa ni kukuza vipaji vya wasanii wa sanaa za jukwaani na sanaa za ufundi.
Programu hi imejipatia umaarufu mkubwa ambapo wasanii hutumia jukwaa la
Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kuonesha vipaji vyao katika sanaa mbalimbali.
Kwa hiyo sisi kama Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni tunasubiri kwa hamu onyesho hilo tunapoumalizia mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023 huku tukisherehekea vipaji halisi vya Kitanzania msimu huu wa sikukuu.
Museum Art Expolsion na Makumbusho ya Taifa ipo wazi kwa wasanii ambao wako tayari kuonyesha kazi zao kwa wananchi na sokoni ndani na nje ya nchi.