Michezo

Sababu za Luiz na Willian kutosafiri pamoja na Coutinho na Fernandinho kurejea England

on

Imezoeleka mara nyingi wachezaji wanaocheza soka katika nchi moja wanaporejea katika Ligi zao baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa zilizopo katika kalenda ya FIFA urudi kwa pamoja, stori iliyokuwa imeingia kwenye headlines ni kuhusiana wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil wanaocheza England kusafiri tofauti.

Willian na David Luiz wanaocheza Chelsea hawajasafiri pamoja na wachezaji wenzao wa timu ya taifa waliokuwa pamoja nao Coutinho wa Liverpool na Fernandinho wa Man City, Luiz na Willian wao wamesafiri peke yao na Coutinho na Fernandinho wamesafiri pamoja tofauti na ilivyozoeleka.

screen-shot-2016-11-17-at-2-35-26-pm

Stori kutoka 101greatgoals.com inaeleza kuwa Chelsea wameacha Willian na Luiz wasafiri na ndege ya kawaida kurejea England kwa sababu hawachezi jumamosi kama ilivyokuwa kwa Coutinho na Fernandinho ambao vilabu vyao vinacheza Jumamosi na Chelsea anacheza Jumapili.

Kitendo hicho cha kusafiri kwa kutumia ndege ya kawaida kinatafsirika kama kutomfurahisha David Luiz kutokana na kutumia account yake ya instagram na kuandika “Too manny flight” akiwa ndani ya ndege ujumbe ambao unaashiria kutofurahishwa utaratibu wa kusafiri kwa kuungaunga na kubadilisha ndege.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments