Michezo

Kipigo cha 5-1 kimefanya FC Bayern Munich imfute kazi kocha

on

Club ya FC Bayern Munich imetangaza rasmi kumfuta kazi akiyekuwa kocha wao Niko Kovac mwenye umri wa miaka 48, siku moja baada ya kufungwa magoli 5-1 dhidi ya Frankfurt.

Kovac raia wa Croatia anaondoka akiwa kashindwa kufikia malengo ya club hiyo na sasa anaondoka Bayern ikiwa nafasi ya nne kwa kuwa na point 18.

Bayern Munich ikiwa chini ya Kovac ndani ya Bundesliga msimu wa 2019/20, imecheza jumla ya mechi 10, imeshinda mechi 5, sare mechi 3 na wamepoteza mechi 2 na kama wangeshinda dhidi ya Frankfurt wagekuwa nafasi ya pili.

Soma na hizi

Tupia Comments