Michezo

Kiukweli Ajax ni wababe tu sio ‘Under Dog’

on

Club ya Ajax ya Uholanzi kwa miaka ya hivi karibuni katika michuano ya UEFA Champions League kwa timu kadhaa imekuwa ikitajwa kama ‘Under Dog’ yaani timu iliyokuwa inapewa nafasi ndogo sana ya kushinda kwa baadhi ya wapinzani wake waliokuwa wanakutana nayo.

Ajax msimu wa 2018/2019 wa UEFA Champions League wamedhihirisha kuwa wao sio timu dhaifu kama baadhi ya watu walivyokuwa wanadhani kuanzia hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League, Ajax baada ya kumfunga Tottenham Hotspurs katika mchezo wa nusu fainali wakiwa ugenini kwa goli la dakika ya 15 kupitia kwa Van De Beek, ndio kauli yao kuwa hakuna timu ya kuiogopa imedhihirika.

Kocha wao kabla ya mchezo huo aliweka wazi kuwa kama wameitoa Real Madrid ambaye ndio Bingwa mtetezi wa michuano hiyo, Juventus ambaye alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kutwaa ta ji hilo basi hakuna timu wanayoweza kuigopa, Ajax unaweza kuwahita wababe kutokana na kuwa na rekodi ya kipekee katika mechi zao za ugenini za michuano ya UEFA Champions League msimu huu.

Ajax katika mechi zao 6 za ugenini za UEFA Champions League msimu huu kuanzia hatua ya makundi hawajapoteza mchezo hata mmoja wa ugenini, hivyo wanastahili kuitwa ni wababe kwa sasa  kwani sio kila timu inaweza fanya hivyo, hizi ndio game za Ajax za ugenini walizocheza, makundi Bayern 1-1 Ajax, Benfica 1-1 Ajax, AEK 0-2 Ajax, 16 bora : Real Madrid 1-4 Ajax, robo: Juventus 1-2 Ajax na nusu fainali leo wameifunga Tottenha, ugenini.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments