Michezo

RIP: Mchezaji wa zamani wa Azam FC Mtibwa na Taifa Stars afariki dunia

on

Familia ya wanamichezo leo imepokea habari za kusikitisha kutoka visiwani Zanzibar kuhusu mchezaji wa zamani wa timu za Azam FC na Mtibwa Sugar Ibrahim Rajab Juma maarufu kwa jina la Jeba ambaye amefariki katika hospitali ya mnazi mmoja.

Jeba hadi mauti yanamkuta alikuwa ni mchezaji wa timu ya Chuoni FC ya kwao Zanzibar na katibu mkuu wa Chuoni FC Mattar Mohamed Suleiman ametoa taarifa za mazishi kuwa Jeba atazikwa kesho.

“Nathibitisha kwamba mchezaji wetu Ibrahim Rajab Juma almaruufu ‘Jeba’ amefariki duniani jioni hii, Ibra alikuwa anaumwa na kwa mara ya mwisho leo mchana alizidiwa na kukimbizwa hospitali ya mnazi mmoja, ndipo alipokutwa na umauti, maziko yatafanyika kesho saa saba mchana kijijini kwao Ndijane”>>>Mattar Mohamed Suleiman

VIDEO: Rekodi mbili atakazoweka Samatta akicheza na kufunga goli UEFA Champions League

Soma na hizi

Tupia Comments