Jumatatu February 11 2019…Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kila mtoto kuanzia chekechekea mpaka kidato cha nne wanapata elimu bure, benki ya UBA Tanzania kupitia kitengo cha UBA Foundation umetoa msaada wa vitabu vya fasihi kwa shule za secokandari za Kimani na Makurunge wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani.
Vitabu hivyo vimepokelewa na Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kimani Mika Bareri na Mkuu wa shule ya sekondari ya Makurunge Hassan Ruheye, Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Mkuu wa shule ya secondary ya Makurunge Hassan Ruheye.
“Ni muhimu kutambua mchango wa makampuni binafsi kama benki ya UBA Tanzania kwa juhudi za dhati za kuunga mkononi serikali yetu katika kuinua sekta ya elimu hapa nchini. Zote tunajua ya kwamba serikali yetu inaongozwa na sera ya serikali ya viwanda. Kwa maana hiyo hatuwezi kuwa na viwanda bila ya kuwa na wasomi wazuri kutoka kwenye shule zetu”>>>>Hassan Ruheye
Ruheye aliongeza “nawaomba benki ya UBA na wadau wengine waendelee kutusaidia kwenye nyaja zingine mbali mbali ili kuendelea kutengeneza mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo kuongeza uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi”.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendashaji wa benki ya UBA Tanzania Flavia Kiyanga alisema “ Sisi benki ya UBA tunaamini jamii iliyoelimika inajengwa kutoka katika shule zenye vifaa vya kufundishia vya kutosha hususani vitabu, ili kuwa na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu kwa shule hizi”.
Benki ya UBA imekuwa kwa muda mrefu ikisaidia sekta ya elimu hapa nchini kwenye Nyanja mbali mbali. Kwa maana hiyo, uongozi wa benki hii ulianzisha kitengo maalum kijulikanacho kama UBA Foundation kwa ajili ya kuendesha zoezi hili. Na kwa kutimizi hili, tumekuwa tukifanya kazi na serikali na naomba nitoe pongezi za dhati kwani serikali imekuwa ikituunga mkono kwa hili.
Kwa upande wake, Ofisa Elimu wilaya ya Kisarawe Patrick Gwivaha alisema kuwa msaada wa vitabu hivi umekuja wakati muafaka wakati shule yetu imekuwa na upungufu wa vitabu na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo”
“Ni ukweli kuwa shule zetu zina uhaba wa vitabu na hasa ukizingatia ya kwamba wilaya yetu imekuwa na ugumu kuifikia maeneo ya mbali na hivyo inakuwa na tatizo la kufikika kwa watu wenye nia njema ya kutupa msaada kwa wenzetu wa benki ya UBA. Vitabu hivi vitajenga hali ya kujisomea kwa watoto wetu na kwa vyovyote vile ufaulu kwenye shule hizi utaongezeka”>>> Gwivaha.
UBUNIFU ULIOFANYWA WAKUTOA ELIMU YA BURE KWA VIJANA WA MIAKA 15 HADI 35