Habari za Mastaa

Mwanasheria wa Meek Mill achukua maamuzi juu ya ubaguzi wa rangi

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Mwanasheria wa rapper Meek Mill atafungua shtaka wiki hii dhidi ya hoteli ya Cosmopolitan kutokana na sakata la ubaguzi wa rangi lilitokea May 26,2018 baada ya rapper huyo kwenda kwa dhumuni la kutazama show.

Mwanasheria Joe Tacopina ameiambia TMZ kuwa kwenye shtaka hilo wataidai kiasi kikubwa cha pesa kutokana na kumchafua rapper huyo ikiwemo kudanganya na kumdhalilisha Meek Mill aliongeza aliapa na kusema kuwa watahakikisha hoteli hiyo inapata adhabu kutokana na kile walichokifanya.

Wiki iliyopita, Meek Mill alizuiliwa kuingia kwenye hoteli ya Cosmopolitan mjini Las Vegas, baada ya ku-post video kupitia ukurasa wake wa instagram na kudai kuwa ni ubaguzi wa rangi umechukua nafasi kubwa kwenye hoteli hiyo huku walinzi wakidai kuwa Millz hakufata utaratibu wa kuingia hivyo watamkamata.

VIDEO: “Ukitualika tunakuja tunafuturu tunapiga selfie tunasepa” Roma Mkatoliki

Soma na hizi

Tupia Comments