fB insta twitter

Siri ya kuzuia udahili vyuo vikuu hadharani

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya yalioandikwa ni huu utafiti wenye kwenye gazeti la Habari leo yenye kichwa ‘Siri ya kuzuia udahili vyuo vikuu hadharani”

Wakati serikali imezuia baadhi ya vyuo vya elimu ya juu kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo wa 2016/2017, kasoro zilizosababisha zuio hilo zimebainika.

Uchunguzi wa gazeti Habari leo uliofanywa kwa  takribani wiki mbili, ulibaini baadhi ya vyuo nchini hutoa elimu bila ya kuzingatia sifa, huku baadhi vikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi kuliko walimu, kutokuwa na maabara na majengo muhimu, kuwa na wanafunzi wasio na sifa, kuwa na wakuu au makamu wakuu wasio na sifa.

Ofisa uhusiano wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Edward Mkaku aliliambia gazeti hilo siku chache zilizopita kuwa serikali kupitia TCU ilikua imeunda Tume Maalum ili kuchunguza uendeshaji wa vyuo vikuu nchini.

Alisema mara baada ya tume hiyo kukamilisha kazi yake, TCU itakua katika nafasi nzuri zaidi ya kueleza kile kilichobainika katika ukaguzi huo na hatua zitazochukuliwa na serikali.

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 25 2016 KUTOKA AYO TV?UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

 

Soma na hizi

Tupia Comments