Habari za Mastaa

Hafsa Kazinja karudi Sekondari….maneno yake nimekuweka hapa

on

.

.

Star wa hit single ya Presha Hafsa Kazinja ambayo alimshirikisha mkali mwingine kutoka B Band maarufu kama Banana Zoro leo alimplify sababu zilizopelekea kuwa kimya kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva.

Akizungumza leo June 26 kwenye AMPLIFAYA ya Clouds FM alisema...’Of course nipo kimya kwenye maradio ila matamasha nafanya kama kawaida naweza nikawa kimya kwenye media lakini kazi zangu bado zinatambulika nje na ndani ya nchi kwa hiyo bado nafanya, lakini kitu ambacho naweza sema kwanini niko busy sasa hivi niliamua kurudi shule kwahiyo nilirudi shule mwaka jana kwa hiyo inataka moyo sana kuanza form one,form two ni (QT) kwa hiyo mwaka jana Mungu akanijalia nikafaulu masomo yangu ya form 1 & 2 sasa hivi niko form 4 nasubiri nimalize maana mtihani wa form 4 sio mchezo

Kwa hiyo pamoja huku nasoma pia nina wimbo wangu mpya siwezi kuuzungumzia ila bado upo katika matayarisho yaani studio’alisema

Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Hafsa Kazinja

Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments