Michezo

Haji Manara afunguka mapokezi ya kombe lao la Ubingwa ‘Tutalipeleka Kidimbwi’

on

Ni Msemaji wa klabu ya Young African, Haji Manara ambae  leo June 22, 2022 alipohojiwa kupitia kituo cha Radio cha Wasafi alizungumzia kuhusu mapokezi ya kombe lao L Ubingwa la ligi kuu (NBC Tanzania Bara).

“Usiku wa Jumapili tunakwenda kidimbwi na Kombe letu kupiga show, wananchi watapata fursa ya kupiga picha na Kombe, tutatengeneza sehemu maalum kutakuwa na ulinzi na jezi zitauzwa kidimbwi itakuwa ni after party ya Yanga,” Msemaji wa Yanga SC

‘Mabingwa mara 14 wa UCL, Real Madrid walifanya sherehe yao ya ubingwa walitumia basi maalum kwaajili ya kudisplay Trophy yao, Man City, Liverpool Timu kubwa kubwa zilitumia na sisi kwa mara ya kwanza Tanzania tumeleta basi kama lile maalum ambalo Hakuna Klabu iliwahi kufanya’

“Hatuta display makombe yetu kwenye mafuso tutadisplay kwenye basi maalum kwa ajili ya shughuli hiyo, hapa navyoongea limeshavuka boda lipo njiani kuja Tanzania,” Msemaji wa Yanga

 

 

Tupia Comments