Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Fid Q ‘Afrika hakuna nchi yenye Wasanii wa Hip Hop kama TZ’

on

Hivi karibuni kumeonekana kuwa na comments nyingi kuhusiana na muziki wa Hip Hop huku wasanii kutokea kwenye Industry hiyo kuonekana kuandika mawazo yao juu ya muziki huo wadau mbalimbali wakilinganisha nani mkali kutokana na hit songs zilizowahi kusikika na ambazo bado zinaskika.

Sasa mwimbaji wa Hip Hop Fid Q ameamua kuandika mawazo yake kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema kuwa Afrika nzima hakuna Nchi yenye wasanii wengi ambapo pia ni wakali kwenye Hip Hop kama Tanzania na kitu kikubwa ambacho kinauangusha muziki huo ni kuchukuliana kawaida tu.

Baada ya mkali huyo kuandika mawazo yake mashabiki waliamua kuandika comments zao kuhusiana na Nicholas alichokiandika Fid Q huku wengine wakidai kuwa wasanii wengi wanakosa heshima ya sanaa huku mwingine alisema anaamini kuwa Audio ikiwa kali kila kitu kingewezekana.

SIMULIZI: MWANAMKE ALIEPATA MIMBA BILA KUKUTANA NA MWANAUME

Soma na hizi

Tupia Comments