Leo ni siku ya maadhimisho ya kitaifa ya haki za binadamu.
Makamu wa Rais Samia Suluhu alikuwa mgeni rasmi katika ufunnguzi wa shughuli hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee, Dar es salaam ikiwa na kauli mbiu ‘Haki zetu, Uhuru wetu daima’.
Akizungumzia mikakati ya Serikali katika kupambana na vitendo vya unyanyasaji kwa jamii Samia amesema “Pamoja na juhudi za Serikali kuboresha mazingira ya upatikanaji na utoaji wa haki za binadamu, matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu yameendelea kuongezeka yakiwemo yale ya mauaji ya kikatili dhidi ya watu wenye ualbino, wanawake wazee, unyanyasaji dhidi ya wanawake , watoto, mauaji ya wanaozaliwa na ulemavu, utekeji nyara pamoja na ajira mbaya”.Samia Suluhu
Kuhusu katiba mpya...”Serikali ya awamu ya tano imepokea kiporo cha mchakato wa katiba ambao haukuweza kukamilika katika awamu iliyopita, napenda kuwahakikishia wananchi tunatambua na kuthamini kazi kubwa iliyofanywa na wananchi walioshiriki hatua ya awali ya ukusanyaji wa maoni ya kuhusu katiba mpya”
“Serikali pia itaendelea pia na mapambano dhidi ya ubadhirifu wa mali za umma, wizi na ufujaji wa fedha, yote haya yatafanyika kwa kuzingatia sheria na haki za binadamu, pia imejipanga kukabiliana na kutokomeza uovu bila kumwonea mtu huruma ambaye anajihusisha na maovu”. Samia Suluhu.
Kampeni maalum za kukuza maadili “Pia nachukua fursa hii kuwaasa Watanzania wenzangu kuanzisha kampeni maalum za kukuza maadili katika ngazi mbalimbali zikiwemo za utumishi wa umma, taasisi za umma na elimu katika nyanja zote”..Samia Suluhu.
Pia Serikali inakusudia kupanua elimu katika ngazi zote kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu kwa kuhakikisha itakuwa bure na kuhakikisha wanafunzi wa elimu ya juu wanapata mikopo, pia huduma za afya zitaboreshwa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.