MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amesema kuwa hakuna mtu, chombo cha serikali wala chama chochote kinachoruhusiwa wala kuwa na mamlaka ya kuahirisha uchaguzi.
Wasira amesema hayo leo Februari 11, 2025 wakati akizungumza katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.
“Ibara ya 41 sehemu ya nne ya katiba inaipa Tume mamlaka ya kutangaza tarehe ya uchaguzi, hakuna chama wala chombo chochote chenye mamlaka ya kuahirisha uchaguzi, ibara ya 42 sehemu ya nne inahusu kama inabidi kusogeza mbele sababu yake lazima iwe vita kwamba Tanzania ipo vitani kwahiyo tunasogeza tarehe mbele ili kumaliza vita,” amesema Wasira.