Kiongozi mpya wa Hezbollah, Sheikh Naïm Qassem, amebainisha siku ya Jumatano Novemba 20 kwamba hakuna makubaliano ya kusitisha mapigano yatakubaliwa ikiwa yatakiuka “uhuru” wa Lebanoni.
Hii ni kujibu nia ya Israel ya kutaka “uhuru wa kuchukua hatua” katika ardhi ya Lebanoni dhidi ya kundi la Kishia, endapo kutakuwa na makubaliano
Kiongozi wa Hezbollah ametoa idhni kutafuta suluhu la kidiplomasia kwa vita vinavyoendelea na Israel.
Hata hivyo, alionya kuwa hataachana na chaguo la kijeshi kukabiliana na majaribio ya Israel ya kukalia kwa mabavu ardhi ya Lebanoni.
Kwenye mahojiano na televisheni, Naïm Qassem ametangaza kwamba Israel “haiwezi kuweka masharti yake” kwa Hezbollah, wakati Washington ilituma mjumbe wake maalum kunyamanzisha silaha.