Shirika la afya duniani WHO na serikali ya Rwanda, wametangaza leo ijumaa kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg, wenye dalili kama Ebola.
Hii ni baada ya lkutangazwa maambukizi mapya katika wiki za hivi karibuni.
Rwanda ilitangaza kisa cha kwanza cha maambukizi ya Marburg mnamo Septemba 27 na kuripoti vifo vya watu 15.
Visa 66 vya maambukizi viliripotiwa kwa jumla, idadi kubwa ya walioathiriwa wakiwa wafanyakazi wa afya waliowahudumia wagonjwa.
Bila matibabu, asilimia 88 ya wagonjwa wanaweza kufariki.
Hakuna chanjo wana tiba dhidi ya Marburg, japo Rwanda imepokea mamia ya dozi za chanjo zinazofanyiwa majaribio tangu mwezi Oktoba.