Wakala wa Neymar Pini Zahavi amesema kuwa hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea juu ya Neymar kuondoka Al Hilal kama ilivyoripotiwa
“Hakuna mazungumzo ya kuondoka Al Hilal, Neymar yupo chini ya mkataba wa miezi sita kuitumikia klabu hiyo na anafuraha sana Al hilal”
“Mimi, Neymar na Baba yake ndio tunaweza kuzungumzia hatua za Neymar kwenye soka sio watu wengine sijui hizo tetesi za kuondoka Al Hilal zimetoka wapi”
Wakala wa Neymar amefunguka hayo baada ya tetesi kuwa klabu ya Santos ya huko Brazil inataka kumsajili mchezaji huyo
Neymar anaona maswali yakiulizwa kuhusu mustakabali wake, baada ya kushindwa kuleta matokeo aliyoyataka katika klabu ya Saudi Pro Leaue Al-Hilal, huku uwezekano wa kuhamia Inter Miami ukijadiliwa – jambo ambalo lingemfanya kuungana tena na Messi kwenye MLS – pamoja na kurejea kwa mizizi yake huko Santos.