Hali ya watu wanaoishi katika makazi huko Gaza imekuwa “mbaya” kutokana na mvua kubwa kunyesha, shirika la Umoja wa Mataifa limesema.
Picha zinazoonyesha barabara yenye watu wengi wakitembea kwenye madimbwi ya maji zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii na Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi.
“Hali katika makazi haifai kuishi kwa kila mtu. Watu hawana chaguo,” shirika hilo liliandika. “Ubinadamu unahitaji kutawala.”
Shirika hilo lilisema karibu watu 884,000 wanaishi katika makazi 154 kote katika eneo hilo, katika ripoti ya hali ya wikendi.
Takriban watu milioni 1.7 wamekimbia makazi yao tangu shambulio la Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba.