Viongozi na wafuasi wa CHADEMA 27 akiwemo Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wamesomewa mashitaka 7 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwemo kumshambulia Askari Magereza.
Hata washitakiwa waliofikishwa mahakamani hapo ni 15 akiwemo mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Meya wa Ubungo, Boniface Jacob na Patrick Assenga (Diwani wa Tabata).
Washitakiwa wamesomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo wamekana kutenda makosa hayo na upelelezi wa kesi haujakamilika.
Washitakiwa wameachiwa kwa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini Bondi ya Sh.Mil 4 kwa kila mmoja.
Washitakiwa wametimiza masharti na kuachiwa, kesi imeahirishwa hadi Aprili 23, 2020.
AMUUA MPENZI WAKE KISA WIVU WA MAPENZI, AJIKATA KOROMEO