Halmashauri ya Kibaha mji imepokea jumla ya pikipiki zipatazo 37 kutoka serikalini kupitia Wizara ya kilimo kwa lengo la kuwawezesha maafisa ugani wa kilimo kutoka kata zote 14 kwa ajili ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi zaidi katika suala la kuwahudumia wakulima na kuleta matokeo chanya katika sekta ya kilimo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John wakati wa halfa ya kukabidhi pikipiki hizo 37 kwa maafisa ugani hao na kuwatka kuhahakikisha kwamba wanaweka misingi ya kuwa na mikakati kabambe katika kuwa na kilimo cha kisasana chenye kuleta tija kwa wakulima.
Mkuu huyo alisema kwamba lengo kubwa la serikali ni kuhakikisha wanaendekea na kufanya juhudi za hali na mali za kuhakikisha inaendelea kuwasajili wakulima wote waweze katika mfumo ambao unatambulika ikiwemo sambamba na kuwapatia pembejeo za kilimo ambazo zitaweza kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Tunapenda kumshukuru kwa dhati Rais wetu wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo pamoja na kutoa vitendea kazi hivi amabvyo ni boda boda 37 kwa maafisa ugani kwa lengo la kuweza kuongeza ufanisi na tija zaidi katika suala zima la kuwahudumia wakulima waweze kuwa na kilimochenye tija katika maeneo yao,”alisema Simon.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha kwamba nia kubwa ya serikali ni kushiikiana bega kwa bega na maafisa ugani katika kuweka mippango endelevu ya kufanya kilimo cha kisasa ambacho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakulima pamoja na wananchi kwa ujumla katika sekta ya kilimo.
Katika hatua nyingine amewaagiza maafisa ugani pamoja na wataalamu wakilimokuhakikisha kwamba wanazitumia vizuri pikipiki hizo kwa kuwafikia walengwa ambao ni wakulima na kwamba dhima kubwa ya serikali ni kuona kunatokea mabadiliko zaidi katika maeneo mbali mbali ya Kibaha mji.