Ikiwa imebaki miezi miwili kufanyika uchaguzi wa Serikaliza mitaa, vitongoji na vijiji kufanyika novemba 27 mwaka huu , halmashauri ya Ifakara Mji Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro imezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la mpiga kura
Mkuu wa Wilaya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya amesema kampeni hiyo inatambulika kama Elimu ya mpiga kura imezinduliwa katika halmashauri hiyo ikiwa ni mandalizi ya kuanza kwa zoezi hilo la uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura linalotarajiwa kuanza octoba 11_octoba 20 mwaka huu katika eneo hilo.
DC Kyobya amesema Sasa ni muda muafaka Kwa Watu mbalimbali mashughuli wakiweno wasanii, viongozi wa dini na kimila kuanza kuhamasha wananchi kujitokeza katika zoezi hilo pindi litakapo anza.
Naye mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Ifakara Mji Zahara Michuzi amesema Kwa Sasa wameanza na makundi maalum kutoa elimu hiyo ikiwemo wajane ,na walemavu .
Amesema halmashauri hiyo itakuwa mfano Kwani viongozi wote wa vijiji na kata tayari wamepewa mwongozo kuhakikisha wanatoa elimu hiyo kwenye Kila sehemu ya mikusanyiko.
Aidha Michuzi amesema wameandaa vipeperushi mbalimbali ambavyo vitasambazwa kwenye nyumba za ibada,huduma za afya,shuleni na maeneo yote yenye mikusanyiko.
Juma Abdalah mkazi wa Lumemo Ifakara amesema uchaguzi wa mwaka huu utakua na hamasa kwani vijana wengi wamekua na uelewa na masuala ya uchaguzi
Anasema hamasa iliyopo imetokana na utendaji kazi wa Viongozi waliopo madarakani ambapo wameona umuhimu wa kupiga kura ili kuchagua kiongozi atakaye leta maendeleo.
Nao viongozi wa vyama vya siasa 14 vya vilivyopo katika eneo hilo kikiwemo,CHADEMA,CCM,UPDP ,CCK ambao walishiriki katika uzinduzi huo wamepongeza kampeni hiyo na kwamba watashirikiana na wanachama wao ili kutoa elimu kufahamu umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura,