Kundi la muqawama wa Palestina Hamas limesema limewaarifu wapatanishi kwamba litashikilia pendekezo lake la awali la kufikia usitishaji vita wa kina, ambao ni pamoja na kuondolewa kwa wanajeshi wa Israel kutoka Gaza na kuwarejesha Wapalestina waliokimbia makazi yao.
Pia ilidai kile ilichokiita “mabadilishano ya kweli ya wafungwa”, ikimaanisha kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina kutoka jela za Israel badala ya mateka wa Israel wanaoshikiliwa huko Gaza.
Hamas iliwasilisha pendekezo la kusitisha mapigano Gaza kwa wapatanishi na Marekani katikati ya mwezi Machi ambalo lilijumuisha kuachiliwa kwa mateka wa Israel ili kubadilishana na uhuru wa wafungwa wa Kipalestina, 100 kati yao wanaotumikia vifungo vya maisha, kulingana na pendekezo lililoonekana na shirika la habari la Reuters.