Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu tayari anaishutumu Hamas kwa kutilia shaka baadhi ya vipengele vya makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza, na kusababisha mgogoro wa dakika za mwisho.
Jambo ambalo Hamas inakanusha
Hamas imepuuzia baadhi ya vipengele vya makubaliano yaliyofikiwa na wapatanishi na Israel katika jaribio la kutaka kupata maafikiano ya dakika za mwisho,” imesema taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.
Baraza la mawaziri la usalama la Israel halitakutana (kuidhinisha mpango huo) hadi wapatanishi waifahamishe Israel kwamba Hamas imekubali vipengele vyote vya mpango huo,” taarifa hiyo inaongeza.
Kwa upande wake, Hamas inakanusha kupinga chochote katika makubaliano hayo: “Tuhuma za Netanyahu kwamba kundi hilo linarudi nyuma kwenye pointi za makubaliano ya kusitisha mapigano hazina msingi,” amesema Sami Abou Zouhri, kiongozi wa kundi la Palestina la Hamas. Israel “inazua mvutano katika wakati muhimu na […] tunatoa wito kwa utawala unaoondoka nchini Marekani na ulz unaoingia kuishinikiza Israeli kutekeleza makubaliano hayo.”