Habari za Mastaa

Harmonize atangaza kiongozi huyu kuwa ni mlezi wa Konge Gang

on

NI Headlines za msanii wa Bongo Fleva, Harmonize ambae leo Octoba 21, 2020 amtangaza kuwa MKuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge kuwa ni mlezi wao wa Konde Gang.

Taarifa hiyo Harmonize aliitoa Kupitia ukurasa wake wa instagram na kuandika ‘Kipekee Kabisa Ningependa Kumshukuru Rais Wetu Dr. JOHN POMBE MAGUFULI kwakututeulia RC kunenge aendeleze pale Walipoishia Viongozi wetu wengine watukufu waliopita’– Harmonize

Katika Harakati Za Kuikuza Na Kuing’arisha DAR ES SALAAM tunaamini Dar es Salaam ni Jiji Kubwa na lenye Dhamana Kubwa mipango mingi Ya Maendeleo, Nitakuwa Sijakosea Sanaa Nikisema Ndio Sura Ya Taifa Hili’- Harmonize

Achilia Mbali Shughuli Nyingi za Kiutendaji Sambamba na hilo kuna Akina Sisi Vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa bila kupepesa Macho tunahitaji mtu wakutuongoza kutusimamia Na kututetea na kuturekebisha pale tunapoteleza Ili tuweze yafikia Malengo yetu ya kuzisaidia familia Zetu Maskini Itoshe Tu Kusema Tumepata Mlezi Na Msimamizi Wa Usalama Pamoja Na Maendeleo Yetu’– Harmonize

Soma na hizi

Tupia Comments