Mix

Harmonize katangazwa kuwa Balozi wa Sayona

on

Kampuni ya Sayona Twist imemtangaza rasmi leo muimbaji wa Bongofleva Rajab Abdul maarufu kama Harmonize kuwa balozi wao kupitia soda za Sayona Twist.

Kuonesha kuwa kampuni hiyo ina imani zaidi ya Harmonize ilimpa fursa ya kubuni chupa ya kinywaji hicho iwe katika muonekano autakao yeye, kitu ambacho walipongeza ubunifu uliopendekezwa na msanii huyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa bidhaa hiyo, Pawan Patel, Mkurugenzi Mtendaji wa Sayona Drinks Limited alisema, “Twist ni kiburudisho chenye ladha nzuri, kinachokupa thamani ya pesa yako. Twist inakuja na ladha saba za kipekee ikiwemo ya pasheni, chungwa, limao, embe, nanasi, tangawizi na ladha ya Cola,”

Pia amebainisha kuwa Kampuni itatangaza ujio wa ladha nyingine za kipekee katika siku za usoni. Aliongeza kuwa, Sayona, imedhamiria kukidhi hitaji la wateja wake ndiyo maana wameendelea kuwa wabunifu na kila mwaka wamekuwa wakitambulisha bidhaa mpya sokoni.

Soma na hizi

Tupia Comments