Harry Maguire analengwa na klabu ya Napoli na Galatasaray, hii kulingana na Ekrem Konur.
Maguire, 31, yuko huru kusaini makubaliano ya awali ya kandarasi na klabu ya ng’ambo kuanzia Januari 1 kutokana na mkataba wake wa sasa Man United kufikia kikomo mwezi Juni, na timu hiyo ya Italia inaongoza kufukuziwa.
Maguire bado hajakubali kuongezwa kwa kandarasi, na pia si mchezaji wa kawaida katika kikosi cha Amorim, jambo linalomaanisha kuwa anaweza kukabiliana na changamoto mpya.
Kocha wa Napoli Antonio Conte tayari amekuwa na furaha kubwa kutoka kwa kiungo Scott McTominay, ambaye alijiunga na klabu hiyo akitokea United majira ya joto yaliyopita, na Maguire anaweza kujiunga na mchezaji mwenzake wa zamani kwa ajili ya kampeni za 2025-26 kama Muitaliano huyo atashinda vita vya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza