Mix

Forbes wamemtaja mchekeshaji anayelipwa zaidi duniani…

on

Mtu wangu wa nguvu kama wewe ni mmoja kati ya mashabiki wa filamu za Comedy basi hii inakuhusu sana, Kutoka nchi Marekani leo September 28, 2016 Jarida la Forbes limetoa list ya wachekeshaji wanaolipwa zaidi duniani.

hart

Good news ni kwamba Comedian Kevin Hart, mwenye miaka 37, amefanikiwa kumuondoa mchekeshaji Jerry Seinfeld kwenye nafasi ya kwanza akiwa kama Comedian analipwa zaidi duniani, akitajwa kuingiza kiasi cha dola za Marekani milioni 87.5 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Forbes, kati ya June 2015 na June 2016, Kevin Hart ameingiza dola milioni 87.5 akimuacha mbali Jerry Seinfeld, aliyeingiza dola milioni 43.5. Mapato haya yametokana na ziara walizofanya, mikataba ya matangazo kwenye makampuni mbalimbali, filamu walizotoa, mauzo ya DVD, Vipindi maalumu vya TV pamoja na mialiko.

Hii ndio list ya wachekeshaji waliotajwa kuingiza pesa zaidi mwaka 2016.

1. Kevin Hart: $87.5million (Tsh. Bilioni 190,973,126,091.28)
2. Jerry Seinfeld: $43.5million (Tsh. Bilioni 94,940,925,000.00)
3. Terry Fator: $21million (Tsh. Bilioni 45,833,550,000.00)
4. Amy Schumer: $17million (Tsh. Bilioni 37,103,350,000.00)
5. Jeff Dunham: $13.5million (Tsh. Bilioni 29,464,425,000.00)
6. Dave Chappelle: $13million (Tsh. Bilioni 28,373,150,000.00)
7. Jim Gaffigan: $12.5million (Tsh. Bilioni 27,281,875,000.00)
8. Gabriel Iglesias: $9.5million (Tsh. Bilioni 20,734,225,000.00)
9. Russell Peters: $9million (Tsh. Bilioni 19,642,950,000.00)
10. John Bishop: $7million (Tsh. Bilioni 15277850000.00)

ULIMISS MUONEKANO WA JIJI LA DAR LEO BAADA YA KUNYESHA MVUA YA MASAA MATANO? TAZAMA VIDEO HII

Soma na hizi

Tupia Comments