Tukiwa bado kwenye headlines za Uchaguzi 2015 nakusogezea hii stori kutoka kwa mgombea Urais kupitia chama cha Ukombozi wa Umma, Hasheem Rungwe.
Ripota wa millardayo.com alipata nafasi ya kupiga stori na mgombea huyo ili kufahamu kuhusu kampeni zake pamoja na kuanzishwa kwa chama chake yaani CHAUMMA.
‘Chama cha Ukombozi wa Umma kilianzishwa mwaka 2012 lakini kilipata usajili 2013 mpaka leo hii kina uongozi wa kudumu na bahati nzuri mimi walinichagua kuwa mwenyekiti wa chama, malengo ya chama chetu ni kuwakomboa watanzania katika hali zao duni’- Hasheem Rungwe
‘Katika msafara wangu wa kampeni zangu nilikuwa na magari mawili katika mikoa mbalimbali na katika kampeni zangu nilikuwa napata watu walikuwa wanakuja na wananisikiliza mimi mgombea wa Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma’- Hasheem Rungwe
‘Idadi ya wadiwani na wabunge katika chama chetu kwanza sisi tumesimamisha wabunge katika mikoa isiyozidi 18 na katika mikoa hiyo yote tuna wabunge na tunao madiwani siwezi kukumbuka idadi yao lakini tunao madiwani Dar es Salaam tuna madiwani Temeke, tuna madiwani Kinondoni’ – Hasheem Rungwe
‘Cha mwisho ambacho ningependa kukisema ni kwamba wale wote waliopitishwa kugombea Urais wanye kwenye mdahalo wazungumzie na asije mtu kumsemea Fulani tunataka wagombea Urais tukutakane kwenye mdahalo ili wananchi wafahamu nini watakachoamua tarehe 25 Octoba, maana nimesikia kuna baadhi ya wagombea wanakwepa mdahalo, kwa hiyo mimi nataka mdahalo hata sasa hivi’- Hasheem Rungwe
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Hasheem Rungwe
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE