Vituko/ Comedy

Kompyuta yake iligoma kufanya kazi…maamuzi aliyochukua ni Stori mtu wangu!!

on

hasiraMara nyingi mtu anapokuwa na hasira anaweza kufanya maamuzi ambayo baadaye anaweza akayajutia, kitendo alichofanya huyu jamaa baada ya kukasirishwa na kompyuta yake huenda hakutarajia angeishia mikononi mwa polisi.

Lucas Hinch amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kuipiga risasi nane kompyuta yake ambayo ilikuwa na matatizo, ambapo akamamua kuipeleka kompyuta hiyo nyuma ya nyumba yake na kuipiga risasi nane.

Maamuzi ya Hinch pia yalichangiwa na kompyuta hiyo kila mara kuonyesha rangi ya bluu na kumchosha ikiwa ni dalili ya kutaka kufa kabisa.

Alichokifanya ni kinyume na sheria, na muda mfupi baadaye alikamatwa na polisi.

mojaInasemekana katika kompyuta hiyo herufi za ctrl+alt+delete zilishindwa kufanya kazi na ndipo alishikwa na hasira na kuamua kulipiza kisasi kwa kuiharibu Kompyuta hiyo hadi kiwango ambacho haiwezi kutumika tena

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenyeTwitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>  Twitter Insta FB  na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments