Habari za Mastaa

Baada ya kutiwa hatiani Asap Rocky atoa ya moyoni

on

Baada ya Mahakama Nchini Sweden kumkuta na hatia Rapper Asap Rocky na kuliweka wazi hilo saa chache zilizopita sasa Rapper huyo ameibuka na kuongea ya moyoni ikiwa ni mara ya kwanza tokea Mahakama imkute na hatia.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Asap Rocky amewashukuru wale wote waliokua nae kwenye kipindi kigumu alichopitia ikiwa pia amesema anasikitishwa na maamuzi yaliyofanywa na Mahakama nchini Sweden ambapo maamuzi hayo yatamuingiza katika kifungo cha jela siku yoyote endapo atavunja sheria nchini humo na hata hivyo imeelezwa kuwa hukumu yake imesogezwa mbele.

“Hakika nimesikitishwa na maamuzi ya leo. Nataka kusema asante tena kwa mashabiki zangu, marafiki na kila mtu ambaye amenionyesha upendo kupitia kipindi hiki kigumu, nitaendelea kusonga mbele naishukuru team yangu, management, mawakili na kila mtu ambaye alitetea haki” >>> aliandika Asap Rocky

Mahakama Nchini Sweden ilitangaza kumkuta na hatia Asap Rocky August 15,2019 na kutoa maamuzi ya kutompa kifungo cha jela na kuamuru alipe fidia ya kiasi cha shilingi Milioni 3 za Kitanzania kwa shabiki aliyemsaobabishia majeraha na kumpiga June 30,2019.

VIDEO: ROSE NDAUKA KUTENGANA NA MZAZI MWENZA ‘NILICHOKA KILA MTU ATAVUNA ALICHOPANDA’, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO.

Soma na hizi

Tupia Comments