Michezo

Huyu ndio golikipa pekee aliyewahi kufunga hat-trick, cheki video ya hat-trick yake hapa …

on

Katika soka kila mchezaji huwa na jukumu lake uwanjani, ataucheze vizuri vipi ila kama hutokuwa ukifanya vizuri jukumu lako uwanjani, basi huwezi kuhesabika kama wewe ni mchezaji mzuri, kwa maana ya kwamba kitu muhimu katika soka ni kumudu nafasi yako uwanjani baada ya hapo ukiwa na vitu vya ziada watu watakupenda ila kama nafasi yako uwanjani inapwaya halafu unaonekana kufanya vizuri nje ya majukumu yako kamwe huwezi wekwa katika kundi la wachezaji bora.

Magolikipa ni watu ambao tumezoea kuwaona wakikaa golini na jukumu lao kubwa ni kulinda goli ili wasifungwe ila ikitokea golikipa akapiga chenga na kufunga goli basi hiyo itakuwa ni uwezo wake wa ziada, November 15 2015 naomba nikusogezee rekodi ya golikipa pekee aliyewahi kufunga hat-trick katika rekodi za soka ambazo zipo katika kitabu cha Guinness.

8640

José Luis Chilavert ndio golikipa pekee aliyewahi kufunga hat-trick katika soka, José Luis Chilavert alizaliwa Paraguay July 27 mwaka 1965 lakini amewahi kucheza soka katika vilabu kadhaa ikiwemo Real Zaragoza, mwaka 1999 ndio aliweka rekodi hiyo baada ya kufunga magoli matatu kupitia mikwaju ya penati, ilikuwa ni mchezo kati ya timu yake ya Vélez Sarsfield dhidi ya Ferro Carril Oeste.

Rekodi ya José Luis Chilavert haikuishia kufunga hat-trick pekee lakini yupo katika nafasi ya pili ya rekodi ya muda wote ya magolikipa wanaoongoza kwa kufunga magoli mengi, amefunga jumla ya magoli 62 nyuma ya golikipa wa kibrazil anayeongoza rekodi hiyo Rogério Ceni anayeongoza kwa kuwa na jumla ya magoli 131. Kama ulikuwa hujui pia José Luis Chilavert ni mtaalam wa mipira ya faulo.

Video ya hat-trick aliyoifunga mwaka 1999

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.

Tupia Comments