Ad

Michezo

Michezo mitano hatari duniani, nimekuwekea na video za michezo yenyewe !

on

Michezo ni moja kati ya vitu vinavyochangia kugawa ajira zaidi duniani, licha ya kuwa mchezo huwafanya watu kuwa matajiri pasipokuwa na elimu, michezo yote duniani inatajwa kuwa sio rahisi kuicheza ila leo December 7 naomba nikusogezee michezo mitano hatari duniani.

1- Mbio za kukimbizana na Ng’ombe (Bull Running) huu ni moja kati ya michezo maarufu sana nchini Hispania, ila ni moja kati ya michezo hatari zaidi, kwani imeshawahi kuchukua uhai wa binadamu licha ya kuwa hata soka tumewahi kuona watu wa kipoteza maisha ila huu ni mchezo ambao hushauriwi kuucheza.

2- Nchi zenye milima yenye barafu mara nyingi huu ndio mchezo unaopendwa kuchezwa ni mgeni barani Afrika na wala sio maarufu kama vile ulivyo mchezo wa soka riadha na michezo mengine, huu unatajwa kuwa mchezo hatari kwani kosa moja tu linaweza gharimu maisha yako, tofauti na mchezo wa soka kosa linaweza sababisha timu kufungwa goli na wala sio kupoteza maisha.

3- Base Jumping huu ni mchezo ambao unachezwa sehemu yenye jengo refu au hata kama ni mlima ila sehemu ambayo wachezaji wa mchezo huo wanaweza kuitumia, ila ajali au bahati mbaya za mchezo huu zinaweza kuchukua maisha ya mwanadamu.

4- Street Luge huu ni mchezo ambao sidhani kama Afrika kuna sehemu wanaucheza huenda ni kutokana na miundombinu ila inatajwa kuwa ni moja kati ya michezo ambayo sio salama sana kushiriki.

5- Heli-skiing huu ni mchezo ambao unachezwa sehemu zenye barafu ila katika mtandao wa wonderslist.com umetajwa kama mchezo hatari kucheza.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments