Waziri wa mipango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Judith Suminwa Tuluka ameteuliwa Jumatatu kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa taifa hilo la Afrika, televisheni ya taifa ilitangaza.
Mchumi huyo, anachukua nafasi ya waziri mkuu kutoka kwa Jean-Michel Sama Lukonde, kufuatia kuchaguliwa tena kwa Rais Felix Tshisekedi mnamo Desemba 20.
Tshisekedi alishinda rasmi kwa asilimia 73.47 na kura ikapita kwa amani katika nchi iliyokumbwa na ghasia na ukosefu wa utulivu kwa muda mrefu.
Upinzani ulitaja kura hiyo kuwa ni udanganyifu.
Upigaji kura uliongezwa rasmi kwa siku moja kutokana na misururu ya vifaa na upigaji kura ulifunguliwa kwa siku kadhaa katika maeneo ya mbali.
Vyama vinavyomuunga mkono Tshisekedi vilipata zaidi ya asilimia 90 ya viti bungeni, hivyo kumruhusu kutunga sheria kwa urahisi.