Michezo

Hatimaye Man City wamekubali kiasi hiki cha pesa kumsajili Sterling

on

Baada ya wiki kadhaa za mazungumzo na ofa tatu kukataliwa, hatimaye vilabu vya Liverpool na Manchester City vimekubaliana kimsingi juu ya ada ya uhamisho wa Winga wa kimataifa wa England – Raheem Sterling.  

Vilabu hivyo vimefikia makubaliano ya ada ya paundi millioni 49 kwa ajili winga huyo mwenye umri wa miaka 20.

Uhamisho huo sasa utakamilika baada ya Sterling kufuzu vipimo vya afya na kukubaliana maslahi binafsi.

Sterling aliomba kuondoka Anfield na alikuwa akiwindwa na vilabu kadhaa kabla ya Man City kuwashinda wengine kwa ofa nzuri.

Mshambuliaji huyo sasa atakuwa mwanasoka ghali zaidi wa timu ya taifa ya England, alikuwa na mkataba na Liverpool mpaka 2017, alikataa ofa ya £100,000 kwa wiki kutoka kwa Liverpool.

Tupia Comments