Miss World Tanzania 2020 Juliana Rugumisa leo hatimae amekabidhiwa zawadi yake ya kushinda nafasi ya pili ya Miss Tanzania 2020.
Juliana alikuwa mshindi wa pili wa Miss Tanzania kwa kushika nafasi hiyo alipaswa kupewa zawadi ya kiwanja kwa mujibu wa waandaaji.
Leo amekabidhiwa hati ya kiwanja hicho kutoka wizara ya ardhi kama alivyokuwa ameahidiwa na wadhamini wa zawadi hiyo Msomi Real Estate.