Top Stories

Hatimaye Trump akubali “nitaondoka”

on

Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwa mara ya kwanza kuwa ataondoka ikulu ya White House iwapo rais mteule, Joe Biden atathibitishwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi wa Marekani.

Hata hivyo Trump bado anaendeleza madai yake kwamba uchaguzi huo kuvurugwa.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari tangu uchaguzi wa Novemba 3, rais Trump alionekana kukaribia kukubali kwamba atahudumu kwa muhula mmoja kabla ya Biden kuapishwa Januari 20 mwakani.

Na baada ya kuulizwa iwapo ataondoka White House, kama jopo la wajumbe maalumu wa uchaguzi la Electoral College litauthibitisha ushindi wa Biden, Trump alikubali kwamba ataondoka na kuongeza kuwa hata waandishi hao wa habari wanajua kwamba ataondoka.

RC TANGA ALIVYOSHTUKIZA HOROHORO NA KUKUTANA NA MADUDU YA WATUMISHI

Soma na hizi

Tupia Comments