Naibu Rais Rigathi Gachagua ameweka matumaini yake kwa Wabunge wanapojiandaa kupiga kura kuhusu hoja yake ya kuondolewa madarakani.
Gachagua amesema anaheshimu na anaamini Bunge litafanya uamuzi sahihi.
Naibu huyo alikuwa akiwahutubia wabunge alipofika mbele ya Bunge kujibu tuhuma zilizowasilishwa kwenye hoja yake ya kuondolewa madarakani.
“Angalia, tafakari, na tumia dhamira yako na ufanye uamuzi yanayofaa,” alisema.
“Ninaheshimu sana Bunge na uwezo wake wa kufanya uamuzi sahihi.” Kiongozi huyo alitetea hatua yake ya kuzungumzia madai hayo siku moja kabla ya kufika mbele ya Bunge.
Gachagua alihutubia taifa katika mahojiano na wanahabari katika makazi yake rasmi ya Karen Jumatatu usiku.