Habari za Mastaa

Siku 7 gerezani Wema Sepetu akiri kupitia wakati mgumu

on

Siku ya June 17,2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru muigizaji Wema Sepetu kupelekwa gerezani siku 7 kutokana na kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa na baada ya kusota jela kwa siku hizo aliachiwa huru na kesi yake iliendelea.

Sasa leo July 4,2019 muigizaji huyo ametumia ukurasa wake wa instagram kuweka wazi kuwa alipitia wakati mgumu sana na hivyo atahitaji mapumziko kutokana na kauli hiyo aliyoiandika imetafsiriwa kuwa hatojihusisha na mitandao ya kijamii kwa muda mrefu baada ya kuandika “Nitawakumbuka”.

“Hakuna kipindi nimepitia wakati mgumu kama hiki wallahy… Nadhani nahitaji Break from everything… I’ll miss you guys…💋” >>>aliandika Wema Sepetu

Wema alidaiwa kutenda kosa la kusambaza video za ngono Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video hizo kupitia akaunti yake ya Instagram pamoja na picha ambazo zilidaiwa kuwa hazina maudhui.

 

VIDEO: ANAEMSOMESHA MTOTO WA MASOGAGE AWAVAA MASTAA “ACHENI MIDOMO, STEVE KATOA HELA”

Soma na hizi

Tupia Comments